Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London.
Wazima
moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba laGrenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.
Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.
Mwandishi wa BBC alisema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka
Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza.
Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo.


Comments