Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 22.06.2017 na Salim Kikeke

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atakaidi hatua ya Antonio Conte na kukataa kuondoka Stamford Bridge, hadi akubaliwe kurudi Atletico Madrid (Daily Star).
Diego Costa amewaambia Atletico Madrid kuwa anataka kurejea Spain. Kutokana na Atletico kufungiwa kusajili, hata akisajiliwa sasa hatoweza kucheza hadi Januari (Sky Sports).
Thibault Courtois hajasaini mkataba mpya, huku Real Madrid wakimnyatia. Kipa huyo wa Chelsea anataka mkataba wa pauni milioni 10 kwa mwaka (The Sun).Real Madrid wanasubiri Manchester United kupanda dau la kumtaka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kabla ya mabingwa hao wa Ulaya kuanza kumfuatilia Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario Gol).
                                                  Kylian Mbappe (kushoto) 
 
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atafikiria kuimarisha safu ya ulinzi kwa kumchukua Leonardo Bonucci kutoka Juventus. Zidane hana mpango wa kusajili mabeki wengine na atatoa nafasi kwa chipukizi ikiwa hawatoafikiana na Juve (Diario Gol).
Hatua ya Ronaldo kubadili mawazo ya kuondoka Real Madrid, imelazimisha Manchester United sasa kuzingatia zaidi usajili wa Alvaro Morata. Jose Mourinho tayari ametenga pauni milioni 60 na wanadhani watamchukua kabla ya mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (The Sun).
Cristiano Ronaldo anafikiria kwenda Paris Saint Germain baada ya kupewa dau na klabu hiyo (Marca).

Comments