Maneno ya Miss TZ 2016 kuhusu Bongo Movie

Miss TZ 2016 Diana Edward amesema kuwa hana nia wala malengo ya kuingia kwenye industry ya uigizaji Bongo maarufu kama Bongo Movie tofauti na warembo wengine wa tasnia ya urembo ambao mara nyingi wamekuwa wakiingia huko baada ya kumaliza muda wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diana ameweka wazi kuwa malengo yake ni
kuweka nguvu kwenye kampeni yake ya dondosha wembe inayolenga kuleta elimu kuhusu ukeketaji nchini hivyo mashabiki wake wasisubiri yeye kujiunga na bongo movie .
“Niweke hili wazi, malengo yangu yapo kwenye Kampeni yangu ya Dondoshawembe si vinginevyo. Bongo movie Hapana Hapana Hapana. filamu za kuelimisha sawa” – Diana Flave.
                                 http://millardayo.com

Comments