Maneno ya Emanuele Palladino: Muacheni Tiote apumzike

Mwili wa Tiote unasafirishwa leo kuelekea Ivory Coast Tiote aliagwa siku ya Jumanne na mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya leo tayari kwa mazish.
Tiote aling'ara vyema akiwa Newcastle
Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivori Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita Emanuele Palladino amewataka waandishi wa
habari na wadau wa soka kuacha kujadili kifo cha mchezaji huyo.
Tiote alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi na klabu yake ya Beijing Enterprises
Ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuungana na familia ya mchezaji huyo katika maombolezo na kuacha kuendelea kuhoji kifo cha mchezaji huyo.




Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015

Comments