Claire na Charlotte Hart
Watoto wake wa kiume, Luke na Ryan, wanasema
walihangaika katika maisha yao yote kuvumilia mwenendo wake wa kupenda kudhibiti kila kitu .
" Hakuwa na jambo la maana la kumfanya aishi kuliko kutuua ," alikieleza kipindi cha Victoria Derbyshire Luke, mwenye umri wa miaka 27.
Mauaji hayo yalitokea siku kadhaa baada ya Bi Hart kuondoka katika nyumba ya familia kufuatia mfarakano baina ya wanandoa hao.
Hart aliwapiga risasi mke na binti yake katika eneo la
dimbwi la kuogelea karibu na eneo la kuegeshea magari kabla ya kujigeuzia bunduki mwenyewe na kujimiminia risasi zilizomuua.
Luke alisema kuwa lilikuwa ni tendo la mwisho la baba yao kuhakikisha familia haiwezi kuishi bila yeye.
Aliacha waraka wa kurasa 12 akisema "kisasi ni chakula baridi kinachogawiwa kwa walaji ".
" Mtu kama baba yetu alikuwa gaidi. Alikuwa anapanga kutuua sote watatu wiki tatu kabla ya kuwauwa ," Alisema Luke.
" Inapokuwa ni baba yako ... hasira huwa isiyoweza kuelezeka. Ni suala gumu sana na la kutisha na vyombo vya habari vililichukulia tukio hilo kama la kawaida, lakini kwetu lilikuwa ni tatizo lililotusumbua kwa muda mrefu .
"alikuwa na namna ya kukufanya ujihisi mnyonge, mtu wa kuhurumiwa na dhaifu na kuhisi unahitaji kusaidiwa ," Alisema Luke.
"alikuwa na utamaduni wa imani kuwa mwanamume ndiye anayeweza kila kitu na watu wengi wanafikiri ni jambo la kawaida.
"http://www.bbc.com
Makaka wawili ambao baba yao alimuua mama yao kwa risasi wamemuelezea baba yao kama "gaidi".
Lance
Hart, mwenye umri wa miaka 57, alimuua mkewe Claire, aliyekuwa na umri
wa miaka 50, pamoja na binti yao Charlotte, aliyekuwa na miaka 19,
kando ya dimbwi la kuogelea (swimming pool) huko Spalding mwezi Julai
mwaka jana.Watoto wake wa kiume, Luke na Ryan, wanasema
walihangaika katika maisha yao yote kuvumilia mwenendo wake wa kupenda kudhibiti kila kitu .
" Hakuwa na jambo la maana la kumfanya aishi kuliko kutuua ," alikieleza kipindi cha Victoria Derbyshire Luke, mwenye umri wa miaka 27.
Mauaji hayo yalitokea siku kadhaa baada ya Bi Hart kuondoka katika nyumba ya familia kufuatia mfarakano baina ya wanandoa hao.
Hart aliwapiga risasi mke na binti yake katika eneo la
dimbwi la kuogelea karibu na eneo la kuegeshea magari kabla ya kujigeuzia bunduki mwenyewe na kujimiminia risasi zilizomuua.
Luke alisema kuwa lilikuwa ni tendo la mwisho la baba yao kuhakikisha familia haiwezi kuishi bila yeye.
Aliacha waraka wa kurasa 12 akisema "kisasi ni chakula baridi kinachogawiwa kwa walaji ".
" Mtu kama baba yetu alikuwa gaidi. Alikuwa anapanga kutuua sote watatu wiki tatu kabla ya kuwauwa ," Alisema Luke.
" Inapokuwa ni baba yako ... hasira huwa isiyoweza kuelezeka. Ni suala gumu sana na la kutisha na vyombo vya habari vililichukulia tukio hilo kama la kawaida, lakini kwetu lilikuwa ni tatizo lililotusumbua kwa muda mrefu .
Luke, Ryan na Charlotte Hart.
Makaka hao wawili walisema kuwa baba yao alidhibiti
nyumba yao kwa kuweka masharti makali ya matumizi ya pesa na kumzuwia
mama yao kupata usaidizi wowote wa kijamii."alikuwa na namna ya kukufanya ujihisi mnyonge, mtu wa kuhurumiwa na dhaifu na kuhisi unahitaji kusaidiwa ," Alisema Luke.

Comments