Helikopta ya polisi yashambulia mahakama ya juu Venezuela

Mahakama ya juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa maguruneti yaliyorushwa kutoka kwa helkopta katika kile rais Nicolas Maduro amekitaja kuwa shambulizi la kigaidi.
Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha helikopta ya polisi ikizunguka mjini kabla ya milio ya risasi na milipuko kusikika.
Polisi ambaye alidaiwa kuiendesha ndege hiyo ya polisi iliyokuwa imeibwa alitoa taarifa ya kupinga serikalia. Hadi sasa hajulikani aliko.Kisa hiki kinajiri baada ya maandamano makubwa kupinga matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Mahakama ya juu nchini Venezuela imeshambuliwa kwa maguruneti yaliyorushwa kutoka kwa helkopta katika kile rais Nicolas Maduro amekitaja kuwa shambulizi la kigaidi.
Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha helikopta ya polisi ikizunguka mjini kabla ya milio ya risasi na milipuko kusikika.
Polisi ambaye alidaiwa kuiendesha ndege hiyo ya polisi iliyokuwa imeibwa alitoa taarifa ya kupinga serikalia. Hadi sasa hajulikani aliko.
Kisa hiki kinajiri baada ya maandamano makubwa kupinga matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Comments