Picha ya mfano ikionyesha waamuzi wakiangalia mchezo kupitia teknolojia ya Var

Shirikisho la soka
duniani Fifa limetetea mfumo mpya wa teknolojia ya Video uliobuniwa
kuwasaidia Marefa kutoa maamuzi sahihi (VAR) kuwa teknolojia hiyo
itafaa sana katika mchezo wa mpira wa miguu siku za mbeleni
Lengo
shirikisho hilo la soka ni kuona teknolojia hiyo inatumika katika
fainali za michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 ambazo pia
zitachezwa Nchini Russia.Rais wa Fifa Gianni Infantino amesema : "Tumeona namna teknolojia hii ya video inavyoweza kuwasaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi uwanjani.
Katika maelezo ya Fifa katika matukio matano yaliyotokea kwenye michuano ya kombe la mabara yakaamuliwa na teknolojia hiyo imeonyesha manne ni ya kuzidi na moja ni la mchezaji kushika mpira.

Comments