Miili 7 ya mabaharia wa Marekani
waliokuwa wametoweka baada ya manoari yao ya jeshi la majini la
Marekani kugongana na meli moja ya mizigo katika pwani ya Japan,
imepatikana.
Maiti hizo zilipatikana ndani ya meli hiyo katika chumba cha kulala ambacho kiliharibika na kujaa maji.- Meli za kivita za Urusi kupitia Uingereza
- China kutengeneza meli inayofanana na 'Titanic'
- Meli ya Japan kuisindikiza meli ya Marekani
Meli ya ACX Crystal iliontkana kugeuka kabl aya jali hiyo kabla ya kuelekea mjini Tokyo Ajali hiyo ilitokea kilomita 100 baharini eneo la Kusini magharibi mwa mji wa bandarini wa Yokosuka, nchini Japan saa nane unusu saa za Japan, jana Jumamosi.
Sehemu moja ya meli hiyo iliharibika kabisa, lakini ikafaulu kurejea katika kambi yake mjini Yokosuka, kwa msaada wa maboti ya jeshi la Marekani.
Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta
Uharibifu kwenye meli ya mizigo ya ACX Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.
Waliojeruhiwa wakiondolewa kutoka meli ya Japan
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.




Comments