Skip to main content
Duniani UTAFITI: Ngozi ya Samaki kutumika kuponya majeraha ya moto
Duniani
Madaktari wa Brazil wameanza kutumia ngozi ya samaki aina ya Tilapia
kutibu majeraha ya moto wakisema ngozi ya aina hiyo ya samaki ina
kiwango kikubwa cha madini ya
collagen na protein ambayo husaidia
majeraha makubwa ya moto kupona haraka.
Wanasayansi hao wameanza rasmi kutumia njia hiyo inayodaiwa kuwa na
ufanisi mkubwa zaidi ya kutumia bendeji za kawaida kwa kuwa ngozi ya
Samaki hao inasaidia kupambana na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia
majeraha ya moto ikiwa na madini yanayosaidia kufuta alama za kuungua
kwa haraka.
Inaelezwa mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 56 waliotibiwa kwa kutumia
ngozi ya Samaki hao wameonesha maendeleo mazuri. Kwa mujibu wa madaktari
hao ngozi ya Nguruwe pia inaweza kutumika kufungia vidonda
vinavyotokana na moto kutokana na kiwango kikubwa cha collage iliyopo
kwenye ngozi hiyo
Comments